Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) akiwalisha samaki chakula kwenye eneo la Lake Side mkoani Mara huku akishuhudiwa na baadhi ya Viongozi na Watendaji wa Wizara yake na Ofisi ya Mkuu wa mkoa huo Desemba 22,2025.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa na Naibu wake Mhe. Ng’wasi Kamani wakivuna samaki kutoka kwenye moja ya vizimba vilivyopo kwenye ziwa Victoria eneo la Lake side mkoani Mara Desemba 22,2025.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (katikati) akimueleza Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba (kulia kwake) fursa zitakazotokana na Bandari ya Uvuvi wakati wa ziara ya Mhe. Dkt. Nchemba bandarini hapo Desemba 19,2025, Kilwa Mkoani Lindi.
Pichani ni sehemu ya pikipiki 381 zilizotolewa na Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa Maafisa Ugani nchini kwenye hafla fupi iliyofanyika Disemba 04,2025 jijini Dar-es-Salaam.
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa (kushoto) akimkabidhi moja ya pikipiki 381 za Maafisa Ugani nchi nzima (wawakilishi waliokaa kwenye pikipiki) Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu-TAMISEMI Prof. Riziki Shemdoe kwenye hafla fupi iliyofanyika Disemba 04,2025 jijini Dar-es-Salaam. Anayeshuhudia (nyuma) ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Ng’wasi Kamani.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Bi. Agnes Meena akimkabidhi Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Balozi Dkt. Bashiru Ally Kakurwa nyaraka za utendaji wa ofisi yake Muda mfupi baada ya kuwasili Makao makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma Novemba 18,2025.