Kuhusu Sekta ya Mifugo

1.0 MAJUKUMU YA IDARA KUU YA MIFUGO

Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa upande wa Sekta ya Mifugo inatekeleza majukumu yafuatayo:-

(i) Kutayarisha, kufanya mapitio na kusimamia utekelezaji wa Sera, Sheria, Mipango na Mikakati ya Kuendeleza Sekta ya Mifugo;

(ii) Kusimamia uendelezaji na matumizi ya ardhi kwa ajili ya ufugaji;

(iii) Kufanya na kuimarisha utafiti katika maeneo mbalimbali ya ufugaji ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za mafunzo na ugani;

(iv) Kuboresha na kuhifadhi kosaafu za mifugo na malisho;

(v) Kuzuia na kudhibiti magonjwa ya wanyama pamoja na wadudu wanaoeneza magonjwa hayo;

(vi) Kuendeleza, kusimamia na kuhamasisha matumizi endelevu ya miundombinu na masoko ya mifugo;

(vii) Kusimamia maendeleo ya sekta ya mifugo kuelekea kwenye uchumi wa viwanda kwa kuboresha mazingira ya uwekezaji, ufanyaji biashara na kuhamasisha uwekezaji wa sekta ya Umma na Binafsi kuwekeza katika sekta ya mifugo;

(viii) Kusimamia uendelezaji, uongezaji wa thamani na upatikanaji wa masoko ya mazao yatokanayo na mifugo;

(ix) Kuimarisha na kujenga ushirika na hasa ule wa vyama vya wafugaji;

(x) Kuendeleza utambuzi, usajili, ufuatiliaji na ustawi wa mifugo;

(xi) Kuongeza upatikanaji na matumizi ya pembejeo na zana za mifugo na matumizi ya wagani;

(xii) Kuboresha utendaji wa Wizara na kuendeleza rasilimali watu; na

(xiii) Kusimamia Wakala, Mashirika na Taasisi za Umma, pamoja na miradi ya mifugo iliyo chini ya Wizara.

2.0 DIRA, DHIMA NA MALENGO

Dira

Kuwa na sekta ya mifugo iliyo shindani na inayochangia maendeleo endelevu ya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Dhima

Kuwezesha ukuaji wa sekta ya mifugo kuwa ya kibiashara na ya kisasa kupitia uandaaji na utekelezaji wa sera, mikakati, miongozo, usimamizi wa sheria, ufuatiliaji na tathmini, kujenga uwezo, weledi na ushirikishaji wa wadau.

Malengo ya Wizara

Ili kufikia Dira iliyowekwa, Wizara inatekeleza mikakati ya malengo yafuatayo kupitia Idara Kuu ya Mifugo (Fungu 99):-

(i) Kupunguza maambukizi ya HIV/AIDS na kuboresha huduma;

(ii) Kuimarisha utekelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa Kupambana na Rushwa;

(iii) Kuzuia na kudhibiti magonjwa ya mifugo;

(iv) Kuwezesha upatikanaji wa masoko ya uhakika ya mifugo na mazao ya mifugo;

(v) Kuongeza uzalishaji na tija kwa mifugo na mazao yake;

(vi) Kuhakikisha Sera, Mikakati na Sheria za Mifugo inaboreshwa na inatekelezwa; na

(vii) Kuimarisha uwezo wa Wizara katika kutoa huduma.

.