Habari

  • WATAALAMU WAHIMIZWA KUINUA MINYORORO YA THAMANI YA MIFUGO

    December 03, 2020

    Wataalamu wa Mifugo wametakiwa kutumia taaluma zao na kushiriki kikamilifu katika kubuni mbinu za kisasa za kuinua viwango vya minyororo ya thamani ya mazao ya Mifugo na Uvuvi ili kuleta tija na kukidhi mahitaji ya uchumi wa viwanda kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

  • ​UTAYARI WA WAFUGAJI KUSHIRIKISHWA KWENYE MIRADI, HUFANYA MIRADI HIYO KUDUMU

    December 03, 2020

    Katibu Mkuu Wizara ya Mifugp na Uvuvi anayeshughulikia Mifugo Prof. Elisante Ole Gabriel amesema wafugaji wanaposhirikishwa katika uchangiaji wa miradi mbalimbali kwa ajili ya mifugo yao wamekuwa wakionyesha utayari na kufanya miradi hiyo kudumu kwa kuwa wanajisikia kuwa sehemu miundombinu hiyo.

  • WAFUGAJI NA WAKULIMA KUNUFAIKA KUPITIA KIWANDA CHA NYAMA NGURU HILLS

    November 30, 2020

    Serikali imesema katika kuboresha na kuondoa migogoro ya wakulima na wafugaji katika maeneo mbalimbali nchini ukiwemo Mkoa wa Morogoro, inasisitiza uwepo wa miradi ambayo itakuwa na manufaa makubwa kwa makundi yote mawili.

  • SERIKALI YAJIPANGA KUIMARISHA SEKTA YA UVUVI NCHINI

    November 30, 2020

    Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi ipo katika mchakato wa kukamilisha Mpango kabambe wa miaka 15 ijayo kuanzia 2021 utakaosimamia sekta ya Uvuvi na kutoa dira ya kulinda rasilimali za uvuvi ili sekta hiyo iweze kutoa mchango mkubwa na endelevu katika pato la taifa.

.