Habari

 • ​ULEGA ATAKA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI KUKOMESHWA NCHINI

  September 01, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amewataka viongozi wa maeneo mbalimbali nchini kuanzia ngazi ya kijiji kuhakikisha wanasimamia haki na amani na kujiepusha na vitendo vya rushwa ili kudhibiti migogoro ya wakulima na wafugaji.

 • ​WAKAGUZI WATAKIWA KUSIMAMIA UBORA WA VYAKULA VYA MIFUGO

  September 01, 2021

  Serikali imewataka wakaguzi wa maeneo ya malisho na rasilimali za vyakula vya mifugo kuhakikisha mifugo inapatiwa vyakula vyenye ubora na stahiki ili kuondokana na madhara ya sumukuvu yanayoweza kuwaathiri walaji wa nyama, mayai, maziwa na bidhaa nyingine za mazao ya mifugo.

 • ​ULEGA ATAKA TAFICO KUJIENDESHA KIBIASHARA KUFIKIA UCHUMI WA BLUU

  September 01, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega amelitaka Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO) kujipanga kibiashara pamoja na kiubia na makampuni binafsi ya uwekezaji mara baada ya kufufuliwa na kuzinduliwa rasmi ili liwe na tija kwa wavuvi na taifa kwa ujumla.

 • ​TAFIRI YATAKIWA KUFANYA TAFITI ZENYE TIJA KWA WAVUVI WADOGO

  September 01, 2021

  Taasisi ya Utafiti wa Uvuvi Tanzania (TAFIRI) imetakiwa kujikita kwenye tafiti zenye tija kwa wavuvi wadogo na kushauri vyema kwenye mamlaka za serikali juu ya njia mbalimbali zikiwemo za kiteknolojia ili sekta ya uvuvi iwe na tija zadi kwa mvuvi mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.

.