Habari

 • ​WAZAZI WAHIMIZWA KUZINGATIA LISHE BORA KWA WATOTO

  September 01, 2021

  Wazazi nchini wamehimizwa kuweka mkazo katika kuwapatia watoto wao lishe bora ikiwemo kuhakikisha wanakunywa maziwa kila wakati ili kuwafanya wawe na afya nzuri itakayowasaidia kufanya vizuri katika masomo yao.

 • ​ULEGA ABAINISHA MIKAKATI YA KUBORESHA MNADA WA PUGU

  September 01, 2021

  Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega (Mb) amesikiliza kero za wafanyabiashara wa mnada wa kimataifa wa Pugu uliopo jijini Dar es Salaam ukiwemo utaratibu wa utoaji wa huduma katika mnada huo, uhaba wa maji, uchakavu wa miundombinu ya kuhifadhia mifugo na ubovu wa eneo la kushusha na kupakia mifugo.

 • ​MATOKEO YA UTAFITI ZIWA TANGANYIKA YAWEKWA WAZI

  September 01, 2021

  Shirika la Chakula na Kilimo ulimwenguni (FAO) kupitia mradi wake wa “FISH4ACP” leo (25.08.2021) limewasilisha matokeo ya utafiti ambao lilifanya kuhusiana na uvuvi wa Ziwa Tanganyika.

 • SERIKALI KUHIMILISHA NG’OMBE MIL. 5 IFIKAPO 2025.

  September 01, 2021

  Wizara ya Mifugo na Uvuvi kupitia sekta yake ya Mifugo ipo mbioni kununua kiwango kikubwa cha gesi aina ya “liquid nitrogen” kutoka kiwanda cha kutengenezea gesi hiyo kinachojulikana kama “Tanzania Oxygen Limited” (TOL)kilichopo Mkoani Dar-es-salaam.

.