Habari

 • TANZANIA, EU KUSHIRIKIANA KUENDELEZA UCHUMI WA BULUU NCHINI

  November 08, 2023

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekutana na Mkurugenzi Mtendaji anayeshughulikia Sera za Uvuvi na Sheria za Masuala ya Bahari kutoka Umoja wa Ulaya (EU), Bi. Charlina Vitcheva kujadiliana namna wanavyoweza kuendelea kushirikiana katika kukuza uchumi wa buluu hapa nchini.

 • ULEGA AKABIDHI BOTI ZA THAMANI YA TSH. BILIONI 1 KWA WAVUVI TANGA

  November 08, 2023

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amekabidhi Boti za kisasa 14 za uvuvi zilizotolewa na Rais, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan zenye thamani ya Shilingi Bilioni 1.2 kwa ajili ya kuwapa wavuvi Mkoani Tanga ili wazitumie kuboresha shughuli zao.

 • ZIARA YA ULEGA THAILAND

  November 08, 2023

  Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega yuko nchini Thailand kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa kujadili changamoto zinazoikabili sekta ya mifugo duniani kutokana na mabadiliko ya kisera, kiuchumi, kijamii na kimazingira.

 • WADAU WAHIMIZWA KUFUGA SAMAKI KUKUZA SEKTA YA UVUVI NCHINI

  November 01, 2023

  Katibu Mkuu, Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Prof. Riziki Shemdoe amewahimiza wadau wa sekta ya uvuvi kujikita katika ufugaji wa viumbe maji ili kusaidia kukuza mchango wa sekta ya uvuvi katika Pato la Taifa kutoka asilimia 1.7 walau kufika mpaka asilimia 5 ifikapo mwaka 2025.

.