WAZIRI LUHAGA MPINA AKUTANA NA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA NCHINI

Imewekwa: Tuesday 13, November 2018

YALIYOJIRI KATIKA KIKAO KAZI CHA WAZIRI Mh. LUHAGA MPINA NA WASINDIKAJI WAKUBWA WA MAZIWA NCHINI.*


Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh.Luhaga Joelson Mpina (Mb) amekutana na Kampuni kubwa za usindikaji wa maziwa nchini (Tanga Fresh, ASAS,MILCOM NA AZAM) leo tarehe 12/11/2018 jijini Dodoma.


Lengo la kikao kazi hicho ilikuwa ni kujadili mikakati ya uongezaji wa Usindikaji wa maziwa kwenye Kampuni kubwa za Maziwa nchini.


Nataka Ifikapo tarehe 12/12/2018 mkakati wa ushirikiano uwe umekamilika na kusainiwa kati ya Kampuni za Wasindikaji wa Maziwa na Dawati la Sekta Binafsi, alisema Mh.Waziri Luhaga Mpina.


Mhe. Mpina aliwaelekeza Wakuu wa Idara na Vitengo kila mtu kwa upande wake kulitumia na kulisimamia dawati katika kutekeleza Mikakati iliyopangwa.


Mkakati huu unaenda kuongeza uzalishaji wa maziwa kwa asilimia 84.7 kwa mwaka, alisema Mpina.


Tunazindua mkakati wa dawati tarehe 15/12/2018 na kwenda kuwakabidhi mitamba 350 kwa wafugaji wa Chama Kikuu-Tanga kama shukurani kwa jitihada za wenzetu wa TADB, Mpina.


# Serikali imefanya jitihada kubwa katika kuongeza uzalishaji wa maziwa ili kusaidia wasindikaji wa maziwa kwa kutekeleza yafuatayo:-
> kuendelea kuboresha vituo vya Uhimilishaji (AI) kwa kutoa mbegu bora.
> ujenzi wa maabara ya (embro transfer) inayozinduliwa mwezi Januari, 2019 Mpwapwa.
> Kudhibiti uingizwaji wa maziwa kutoka Nje kwa kuongeza kodi ili kulinda viwanda vya ndani.
> Serikali imetoa hekta 10,000 Ruvu kwa ajili ya ufugaji wa ng’ombe wa maziwa.
> Serikali itasambaza Madume kwa bei ya ruzuku.
> Tumehamasisha viwanda vya vyakula vya mifugo.

Tutahakikisha katika maeneo ya wafugaji Huduma zote za Ugani zitatolewa na wataalamu wetu na zitawafikia kwa ajili ya kujua uzalishaji wa Mifugo, alisema Mpina.

Mhe Waziri aliwasisitizia Wawekezaji kuwa, kuna vijana wamemaliza vyuo mbalimbali vya Mifugo na hawana ajira watumieni kuongeza Uzalishaji.


Naye kwa upande wake Mkurugenzi Kampuni ya Tanga Fresh,Bw. Michael Karata alimpongeza Mhe. Waziri Mpina kwa jitihada za kuwaunga mkono alizozichukua katika sekta hiyo mpaka sasa.

Kampuni hiyo ya maziwa ya Tanga Fresh iliahidi kuongeza Usindikaji wa Maziwa kutoka Lita 45,000 hadi 90,000 kwa siku ifikapo Disemba 2018.


Vilevile Mkurugenzi wa ASAS Bw. Fuad Abri alisema,tunashukuru na kuunga mkono Sekta hii ya maziwa na ndoto ya ASAS sio kuuza Tanzania bali kuuza nje ya Tanzania.


Tutahakikisha tunaachana na maziwa ya unga na kutumia maziwa ghafi alisisitiza Mkurugenzi wa Mahusino, Bw. Hussein Ally AZAM.


Kwa upande wake Meneja wa TADB Kanda ya Kati Bw. George Nyamrunda alisema, watakopesha wafugaji na wadau katika kuongeza uzalishaji wa maziwa.


Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Profesa Elisante Ole Gabriel naye alisisitiza, Wakurugenzi watumie muda wao kulijua kwa undani na kulisaidia dawati la Sekta binafsi ili liweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

Aidha Prof.Gabriel alilitaka Dawati hilo kushirikiana kwa karibu na Kitengo cha Mawasiliano ili kuelimisha umma juu ya utekelezaji wa shughuli zifanywazo na dawati hilo.

Pia Katibu Mkuu Prof.Gabriel aliiomba Benki ya Maendeleo ya Kilimo Nchini (TADB)iangalie uwezekano wa kusaidia ununuzi wa vifaa vya Kitengo cha Mawasiliano ili kufanikisha utekelezwaji wa mkakati wa Mawasiliano wa Wizara.

.