Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
WAWEKEZAJI WATAKIWA KUGEUKIA FURSA YA KILIMO CHA MBEGU ZA MALISHO YA MIFUGO

Serikali imewataka wadau wa uwekezaji nchini kugeukia Sekta ya Mifugo hasa katika kutumia fursa ya changamoto ya uhaba wa mbegu za malisho ambayo mahitaji yake ni zaidiya tani milioni 7 kulinganisha uzalishaji wa sasa wa tani 127 pekee.
Rai hiyo ilitolewa na Katibu Mkuuwa Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Elisante Ole Gabriel wakati akifungua warsha maalum ya wadau wa uzalishaji mbegu za malisho hapa nchiniMkoani Morogoro 12, Mei 2021.
Alisema kuwa takwimu zinaonyeshakiwango cha uzalishaji wa mbegu ni mdogo ukilinganisha na mahitaji yake na kwamba kama wawekezaji wakigeuza changamoto hiyo kuwa fursa inasadia kwa kiasi kikubwa kuongeza uzalishaji.
“Mahitaji ya mbegu za malisho Tanzania ni tani milioni 7 lakini kiwango chambegu kilichozalishwa kwa mwaka 2019/20 ni tani 127 maana yake ni kwamba kuna uhaba mkubwa sana ivyo changamoto hiyo tuichukulie kama fursa ya uwekezaji katika sekta hiyo” alisema Prof Gabriel.
Kadharika alisema Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuviitaendelea kushirikiana na wadau wa maendeleo, makampuni na watu binafsi wenye nia ya kuzalisha mbegu bora za malisho, kufanya kazi hii kibiashara kwa kuwapa mwongozo unaostahili.
Alibainisha kuwa lengo ni kufanikisha juhudi hizi za Serikali hasa kujiletea faida za kiuchumi kupitia uwepo wa fursa ya wingi wa mifugo nchini na hata kuuza malisho katika mataifa mengine.
“Hii si tu kwamba itainua uchumi wa mtu binafsi bali italipatia Taifa fedha za kigeni, hasa tukizingatia kuwa wananchi wanaweza kutumia fursa ya ardhi iliyopo kuzalisha malisho kibiashara kama wanavyo zalisha mazao ya chakula”. alisema Prof. Gabriel
Kwa upande wake Mkurugenzi Idara ya Utafiti Mafunzo na huduma za Ugani, Dkt. Angello Mwilawa alisema lengo la warsha hiyo ni kuhakikisha tafiti zilizofanyika kubaini mbegu bora za malisho zinawafikia wafugaji wadogo kwenye mashamba yao.
Alisema zipo mbegu ambazo zimekuwa rahisi kuwafikia wafugaji kama mbegu aina ya Nyasi, mikunde inayotaambaa na mikunde jamii ya miti malisho ambazo zipo katika makundu tofauti ambazo pia mahitaji ya msingi katika mashamba ya malisho.
“Tunaona kuna fursa kubwa ya uzalishaji wambegu endelevu na hapa tunazungumzia mbegu mafungu matatu ambazo hizo tunaangalia ni namna gani tunaongeza uzalishaji hapa nchini” alisema Dkt. Mwilawa.