WANAFUNZI MIFUGO NA UVUVI KUNUFAIKA NA PROGRAM YA MAFUNZO NJE YA NCHI.

Imewekwa: Wednesday 01, November 2023

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi leo Oktoba 17,2023 amekutana na ujumbe kutoka Shirika la kimataifa la Bixter linalojishughulisha na uratibu wa mafunzo kwa vitendo katika nyanja za Mifugo na Uvuvi kwa wanafunzi kutoka barani Afrika na Asia.

Ujumbe wa Shirika hilo ambalo hupokea wanafunzi na wahitimu kutoka kwenye nchi zinazoendelea na kuwapeleka kupata elimu kwa vitendo katika nchi za Denmark, Ujerumani, Sweden Norway na Poland ulifika makao makuu ya Wizara hiyo yaliyopo eneo la Mtumba jijini Dodoma ambapo uliongozwa na Mwanzilishi na Mkurugenzi wake Bi. Nataliya Jorgensen.

Akizungumza mara baada ya kikao kifupi baina ya ujumbe huo na baadhi ya wakurugenzi na wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Dkt. Mushi amebainisha kuwa ujio wa shirika hilo utakuwa ni fursa kwa wanafunzi na wahitimu wa vyuo vilivyopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi ambapo watapata nafasi ya kwenda kufanya mafunzo yao kwa vitendo kwenye mashamba na viwanda vinavyojishughulisha na uchakataji wa mazao ya mifugo na Uvuvi.

"Mpaka sasa Shirika hili kwa kushirikiana na Programu ya kuwaandaa vijana katika nyanja za kilimo, mifugo na uvuvi (SUGECO) wameshapeleka vijana wa kitanzania 480 hivyo tunaamini hata vijana wetu wakienda huko watarejea kuwa msaada mkubwa kwenye kuendeleza sekta za Mifugo na Uvuvi nchini na hivyo tumekubaliana tuwe na MoU kati ya Wizara, SUGECO na Bixter ili kurasimisha ushirikiano wetu" Ameongezea Dkt. Mushi." Ameongezea Dkt. Mushi.

.