Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
ULEGA ATEMBELEA MIRADI YA UFUGAJI SAMAKI KATIKA VIZIMBA, MWANZA
ULEGA ATEMBELEA MIRADI YA UFUGAJI SAMAKI KATIKA VIZIMBA, MWANZA
Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega ameonesha kufurahishwa na vijana wanaofanya miradi ya ufugaji wa samaki katika vizimba jijini Mwanza baada kuwatembelea na kuona maendeleo mazuri yaliyofikiwa na vijana hao tangu walivyokabidhiwa vizimba hivyo na Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, mwezi Januari 30, 2024.
Ulega ametembelea vijana hao mapema leo Aprili 30, 2024 ambapo aliwapongeza vijana hao kwa kazi nzuri waliyoanza kuifanya huku akiwatia shime kuendelea kuwa imara kwani siku zote mwanzo ni mgumu lakini kwa hatua waliyofikia imeonesha matumaini makubwa kwao na kwa serikali pia.
Aliwaeleza vijana hao kuwa maono ya Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kujenga kesho iliyobora kwa vijana hivyo mradi huo wa vizimba ni sehemu ya hatua anazoendelea kuzichukua katika kuhakikisha vijana wanajikomboa kimaisha kupitia fursa zilizopo kwenye sekta ya uvuvi.
Aliongeza kwa kuwataka vijana hao kuongeza bidii katika ufugaji wao kwani watapokuwa wamefanya vyema itakuwa ndio mwanzo wa kuvutia uwekezaji zaidi katika tasnia hiyo ya ufugaji samaki kwenye vizimba.
Aidha, Vijana hao wanaofanya ufugaji katika maeneo Kisoko, Nyegezi na Tangabuye, Ilemela walimueleza Waziri Ulega kuwa katika kila Kizimba kimoja wanatarajia kupata mavuno ya kuanzia Tani 5 hadi 6 na kwa kila kizimba wanatarajia kupata kati ya shilingi Milioni 28 hadi 30.
Waziri Ulega aliendelea kusema kuwa katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wataendelea kuwekeza katika miradi hiyo ikiwemo kuwatafutia boti ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa urahisi zaidi.