Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
ULEGA AALIKA WAWEKEZAJI KUUNGA MKONO BBT

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega amewaomba Wadau na Wawekezaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kuwekeza katika programu ya BBT ili kuunga mkono jitihada za Mhe. Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan za kuinua wanawake na vijana kupitia sekta za mifugo na uvuvi.
Waziri Ulega alitoa wito huo wakati wa hafla fupi ya kujenga uhusiano na ushirikiano baina ya Wadau na Wawekezaji wa ndani na nje ya nchi iliyoandaliwa na Shirika la Heifer International ambayo ilifanyika jijini Dar es Salaam kando ya Mkutano wa Jukwaa la Mifumo ya Chakula Barani Afrika (AGRF).
Wakati akiongea na wadau na wawekezaji mbalimbali walioshiriki hafla hiyo, Mhe. Ulega alisema kuwa BBT ni programu ya kielelezo ya Mhe. Rais, Dkt Samia na mpaka sasa Serikali imeshawekeza kiasi cha shilingi bilioni 20.3, lakini ili programu hiyo iweze kufanikiwa na kuwa endelevu inahitaji kuungwa mkono na wadau kwa namna mbalimbali ikiwemo fedha na tekinolojia.
"BBT ni programu ya kielelezo ya Rais, Dkt. Samia na wadau mbalimbali wakiwemo Wadau wa maendeleo na sekta Binafsi wameonesha nia ya kuiunga mkono wakiwemo heifer international, nitumie nafasi hii kuwaomba Wadau wa maendeleo na sekta Binafsi mjitokeze kwa wingi katika kuunga mkono jitihada hizi za Mhe. Rais za kuwainua wanawake na vijana," alisema
Aidha, alitumia nafasi hiyo pia kulishukuru Shirika la Heifer International kwa kuendelea kuwa miongoni mwa wadau muhimu katika sekta ya mifugo, huku akiwapongeza kwa mradi wao wa Kopa Ng'ombe, Lipa Maziwa ambao ng'ombe takriban 300, 000 walikopeshwa kwa wafugaji wadogo wa ng'ombe wa maziwa hapa nchini.