Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
​TAASISI ZATAKIWA KUTUMIA VYEMA MAPATO YA NDANI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Sekta ya Mifugo Dkt. Daniel Mushi ametoa rai kwa taasisi zilizo chini ya wizara hiyo kufanya kazi kwa bidii na kujijengea uwezo wa kujipatia vyombo vya kazi ili wafanye kazi kwa ufasaha.
Dkt. Mushi amebainisha hayo (10.07.2023) wakati alipokuwa akizindua gari aina ya Toyota Hilux Pickup Double Cabin 2 GD STD Manual iliyonunuliwa na Bodi ya Nyama nchini (TMB) kwa thamani ya Shilingi Milioni 99.9.
Akizungumza katika ofisi za bodi hiyo jijini Dodoma amesema ni vyema taasisi za Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuwa na matumizi mazuri ya fedha kwa kununua vifaa mbalimbali vya kutendea kazi badala ya kufanya matumizi ya fedha yasiyo na tija.
Kwa upande wake Kaimu Msajili wa Bodi ya Nyama Bw. John Chassama amesema gari hilo wamenunua kwa mapato ya ndani ambapo wamepanga kulipeleka Kanda ya Arusha na kwamba mipango ni kuhakikisha kila kanda inakuwa na gari ili kuboresha utendaji kazi.
Bw. Chassama amesema pamoja na ununuzi wa magari mpango wa bodi ni kuimarisha ofisi za kanda kwa kununua vifaa vingine zikiwemo kompyuta ili kusogeza karibu huduma kwa wadau kwa kutumia teknolojia ya kisasa.