Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI JULAI HADI DESEMBA 2024 YAJADILIWA

TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA BAJETI JULAI HADI DESEMBA 2024 YAJADILIWA
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo wakiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo Mhe. Deodatus Mwanyika wamepokea na kujadili Taarifa ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara kwa kipindi cha kuanzia Tarehe 1 Julai - 31 Desemba 2024.
Taarifa hiyo imewasilishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi leo tarehe 14 Januari, 2025 katika ukumbi uliopo Ofisi za Bunge Jijini Dodoma ikiongozwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Dkt. Ashatu Kijaji, akiambatana na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Prof. Riziki Shemdoe pamoja na watendaji wake.
Sambamba na hilo Wizara imewasilisha na kufanya mapitio ya taarifa ya utekelezaji wa maazimio ya Bunge yaliyotokana na Taarifa ya Mwaka wa Shughuli za Kamati iliyowasilishwa Bungeni Februari, 2024.