SIJARIDHISHWA NA KASI YA UJENZI - DKT. TAMATAMAH.

Imewekwa: Tuesday 21, July 2020

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) Dkt. Rashid Tamatamah hajaridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa Jeongo la Utawala la Ofisi ya Hifadhi ya Bahari na Maeneo Tengefu (MPRU) unaoendelea katika Kisiwa cha Mafia.

Dkt. Tamatamah aliyasema hayo baada ya kukagua kazi za ujenzi zinazoendelea ambapo hakuridhishwa na kasi ya ujenzi kwani haiendani na muda uliotumika kwa mujibu wa mkataba.

"Sijaridhishwa na kasi ya ujenzi niliyoikuta hapa hivyo ninakuagiza mkandarasi kuhakikisha unazingatia ratiba na muda uliopangwa kulingana na mkataba" Alisisitiza Dkt. Tamatamah.

Jengo hilo linasimamiwa na mkandarasi mwelekezi "Y&P architects" linatarajiwa kutumiwa na MPRU kama ofisi mara baada ya kukamilika kwake ambapo litasaidia kuongeza ufanisi wa taasisi hiyo.

.