Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
SERIKALI YA DKT. SAMIA YAENDELEA KUWAINUA WAVUVI

Katika hatua za kutekeleza mikakati ya kujenga na kuboresha uwezo wa wavuvi kufanya kazi zao kwa uhakika na kuimarisha usalama wao, Serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan imegawa kwa wavuvi vifaa vya kujiokolea ili waepukane na matatizo ya kuzama baharini.
Hayo yalifahamika wakati Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega akigawa vifaa hivyo kwa wavuvi wa Kizimkazi, Mkoa wa Kusini, Zanzibar Juni 22, 2023.
Wakati wa hafla fupi ya ugawaji wa vifaa hivyo, Mhe. Ulega alisema kuwa utekelezaji na ugawaji wa vifaa hivyo kutoka kwa Serikali ni msukumo katika utekelezaji wa Sera ya Uchumi wa Buluu.
"Vifaa hivi tunavyowakabidhi leo vitawasaidia kuboresha shughuli zenu lakini pia kuwawezesha kufanya uvuvi salama na kujiokoa na kuzama majini," alisema
Aidha, Mhe. Ulega alitoa wito kwa wavuvi hao kuhakikisha wanahifadhi na kuyatunza mazingira ya Bahari ili kuwa na uvuvi endelevu na kutekeleza wa sera ya uchumi wa buluu.
Katika hafla hiyo, Wavuvi walikabidhiwa Makoti ya kujiokolea Mia moja (100), Gps Nne (4) ambapo vifaa hivyo vitatumiwa na vyombo 25.