PROF. SHEMDOE ASISITIZA MAMBO SITA YA KUZINGAZIA KATIKA UANDAAJI WA MRADI WA MAZIWA

Imewekwa: Thursday 14, September 2023

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi Prof. Riziki Shemdoe leo tarehe 13 Sept 2023, ameshiriki ufunguzi wa mkutano unaoandaa andiko la mradi wa kuongeza uzalishaji wa maziwa huko Kigali nchini Rwanda kwa kuzingatia mabadiliko ya tabia nchi, na kupunguza gesi joto kwa nchi nne za Africa Mashariki (Kenya, Rwanda, Tanzania, na Uganda)

Aidha, Mkutano huo wa siku tatu unaofanyika nchini humo, Prof.Shemdoe amewaelekeza washiriki kufikiria kuelekeza fedha na utaalam wa mradi huo kwa Upande wa Tanzania katika maeneo sita ambayo ni pamoja na BBT-LIFE, kuongeza ushiriki wa vijana na wanawake, kuongeza utajiri kwa wadau, kuongeza uzalishaji, kuimarisha mradi wa kopa ng'ombe lipa maziwa na kutilia mkazo suala la "Livestock Guest House".

.