Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
POLAND YAKOSHWA NA USHIRIKIANO WAKE NA TANZANIA
POLAND YAKOSHWA NA USHIRIKIANO WAKE NA TANZANIA
Nchi ya Poland imefurahishwa na ushirikiano uliopo baina yake na Tanzania ambapo imeahidikuendeleza ushirikiano huo ili kuboresha miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ile inayohusu sekta ya mifugo nchini.
Hayo yamesemwa leo (22.06.2021) na Naibu Waziri wa mambo ya Nje wa nchi hiyo, Pawel Jablonsiki mara baada ya kufika na kukagua maabara ya uchunguzi wa magonjwa ya mifugo iliyopo kwenye taasisi ya Wakala ya Mafunzo ya Mifugo (LITA) kampasi ya Tengeru iliyopo jijini Arusha.
“Nimefurahishwa sana na kazi kubwa iliyofanyika hapa na nina imani miradi mingine inayotekelezwa kwa ushirikiano baina yaTanzania na Poland itaendelea kutekelezwa kwa mafanikio makubwa” Amesema Jablonsiki.
Balozi huyo wa Poland amesema kuwa Uhusiano mzuri uliopo baina ya nchi yake na Poland ndio kitu kikubwa ambacho pande hizo mbili zitaendelea kujivunia daima ambapo ameonesha kutambua na kuthamini mchango wa Tanganyika kwa nchi hiyo wakati wa Vita kuu ya pili ya dunia.
“Ninaomba Katibu Mkuu unifikishie salamu kwa Waziri kwa sababu ninatambua kazi kubwa anayoifanya katika kukuza sekta ya mifugo nchini na sisi kama Poland tutaendelea kutoa ushirikiano wa kutosha katika kutekeleza miradi mbalimbali inayolenga kuboresha sekta hiyo hapa nchini” Ameongeza Jablonsiki.
Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof. Elisante Ole Gabriel ambaye alimwakilisha Waziri wa Mifugo na Uvuvi ameishukuru nchi ya Poland kwa mchango wao katika kukuza sekta ya mifugo nchini ambapo alimuomba Waziri huyo kuihakikishia Serikali ya Poland kuwa Wizara yake ipo tayari kuendelea kushirikiana kwa ukaribu na nchi hiyo.
“Lakini jambo moja ambalo Mhe. waziri wangu amesema nikuombe ni kwamba sasa maabarazimeshakarabatiwa zikiwa na vifaa vya kisasa hivyo pale ambapo hali ya korona itakapokuwanzuri tungependa kuwepo na mpango wa kubadilishanawanafunzi baina ya Tanzania na Poland” Ameongeza Prof. Ole Gabriel.
Aidha Prof. Ole Gabriel ameainisha kuwa maabara hizo zilizoboreshwa kwa msaada wa nchi ya Poland zitawasaidia wanafunzi kujifunza kwa vitendo kuhusu masuala mbalimbali ya kitaalam yanayohusu mifugo nchini ambapo ameahidi kuitunza miundombinu hiyo ili iweze kutumika kwa muda mrefu zaidi.
Kwa upande wake Mtendaji Mkuu wa Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) Dkt. Pius Mwambene amesema kuwa nchi ya Poland imetoa ufadhili kwenye miradi 6 ya taasisi hiyo ambapo miongoni mwa miradi hiyo ni huo wa uboreshwaji wa maabara za mafunzo za taasisi hiyo kampasi ya Tengeru.
“Mbali na maabara hizo, Wakala ya Mafunzo ya Mifugo nchini (LITA) inatarajiwa kuwa na vituo vitatu vya umahiri ambapo kituo cha Tengeru kitakuwa kikihusiana na masuala ya maziwa, kituo cha Mabuki mkoani Mwanza kitajihusisha na masuala ya nyama na kituo cha Morogoro kitahusiana na masuala ya ngozi” Amesisitiza Dkt. Mwambene.
Wakala ya Mafunzo ya Mifugo Tanzania (LITA) imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa wataalam wa mifugo nchini lengo likiwa ni kuboresha sekta hiyo na kuifanya iendelee kutekelezwa kwa tija.