Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Maafisa uvuvi kuweka hadharani tozo za samaki

Imewekwa: Monday 27, August 2018

ULEGA AAGIZA TOZO ZA SAMAKI NA MAZAO YA UVUVI KUWEKWA WAZI NCHINI, MATUMIZI YA NYAVU HARAMU YAKOMA

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amewaagiza Maafisa uvuvi kuweka hadharani tozo za samaki pamoja na mazao ya uvuvi kwa wafanyabiashara wa bidhaa hizo.

Ulega amesema hayo leo katika soko la samaki la kimataifa la Kirumba jijini Mwanza wakati wa ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali ya mifugo na uvuvi.

Ulega ameeleza kuwa viongozi husika lazima wajue na kutambua majukumu yao bila kusubiri Waziri kuja kukagua maendeleo ya masoko. Na amewataka na maafisa na wafanyabiashara kukaa na kupanga mikakati ya kuongeza mapato ya Serikali.

Aidha ameagiza kuwa masoko yote ya samaki yaweke wazi tozo ambazo mfanyabiashara anatakiwa kulipa pindi wanunuapo bidhaa.

Pia Naibu Waziri amewataka Maafisa kutembelea masoko kila wiki ili kujua maendeleo ya masoko, Kuhusu udhibiti wa uvuvi haramu Ulega amewapongeza wavuvi kwa kutii sheria bila shuruti kwani hakuna nyavu haramu iliyokamatwa katika ukanda wa ziwa Viktoria na Kayenze.

Pia amewashauri wafanyabiashara kujua tozo wanazotakiwa kutoa kabla ya kununua mizigo kwani itawasaidia sana katika ufanyaji wao wa biashara kwa kutambua kiasi wanachotakiwa kulipa kama tozo kuliko kutoa tozo bila kujua nj kiasi gani wanatakiwa kulipa.

Kwa upande wao wavuvi pamoja na wafanyabiasha ra wameishukuru serikali kwani kwa sasa samaki wanapatika tofauti na mwaka jana na wamewataka maafisa kushirikiana nao ili kuweza kufikia malengo ya juu zaidi.

.