Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
MCHAKATO WA KUPITIA UPYA SERA YA MIFUGO WAIVA, INALENGA KUONGEZA KIPATO KWA WATANZANIA WANAOTEGEMEA MIFUGO.

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki amesema, sekta ya mifugo ina nafasi kubwa katika kujenga uchumi imara wa Taifa, kuongeza kipato kwa Watanzania wanaotegemea mifugo, kutoa fursa za ajira na kuhifadhi rasilimali za Taifa.
Ndaki alisema hayo Nov 9, 2021, mjini Morogoro kwenye hotuba ya ufunguzi kikao kazi cha wadau mbalimbali kutoka taasisi za Serikali, wizara na sekta binafsi wanaohusika na sekta ya mifugo kwa ajili ya mapitio ya sera ya mifugo ya mwaka 2006, ambayo iliyosomwa kwa niaba yake na Kaimu Katibu Mkuu (Mifugo), Amosy Zephania.
Waziri Ndaki alisema, mchakato wa kupitia sera ya mifugo, Serikali imewashirikisha wadau wa sekta hiyo ili watoe mapendekezo madhubuti yatakayowezesha sekta ya mifugo kutoa mchango kikamilifu kwa maendeleo ya watu na ukuaji wa uchumi kwa ujumla.
Hivyo aliwataka Watendaji wa wizara hiyo kuhakikisha kuwa maazimio yaliyowasilishwa katika mkutano wa wadau wa sekta ya mifugo uliofanyika Septemba 7 na 8, mwaka huu (2021) ambayo yanabainisha changamoto za kisera katika sekta ya mifugo yazingatiwe katika mapitio ya sasa ya sera.
Waziri huyo pia aliwahakikishia wadau wa sekta binafsi kuwa, Serikali ipo pamoja nao katika kila hatua ya kuelekea Tanzania ya Viwanda inayotarajiwa na kwamba mapitio ya sera hiyo ni miongoni mwa dhima ya nchi ya kuimarisha viwanda.
“Serikali inaendelea kuweka mazingira mazuri ya uwekezaji na ufanyaji biashara katika sekta ya mifugo ili iweze kukua kwa kasi na kuwa shindani kikanda na kimataifa” alisema Waziri Ndaki.
Pia Waziri huyo aliwashukuru wadau wote wakiwemo wabia wa maendeleo hususani kundi la wafadhili wa Kilimo kwa ujumla ambalo Shirika la Chakula na Kilimo la Umoja wa Mataifa (FAO), ni sehemu kwenye kundi hilo.
Waziri Ndaki pia alitoa wito kwa wafadhili kuendelea kuunga mkono Serikali ya awamu ya sita ambayo ina matarajio makubwa kuona sekta ya mifugo inachangia ipasavyo katika kupunguza umaskini kwa Watanzania hususani wanawake, vijana na watu waushui vijijiji.
Naye Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango wa Wizara hiyo, Deudedit Kaganda alisema mapitio ya sera ya mifugo ya mwaka 2006 ukusanyaji wa maoni ya wadau wa mazao ya mifugo nchini na kuhuisha sera hiyo kwa wadau umeanza Novemba 9, mwaka huuna kuendelea mikoa mingine hadi Aprili 2022.
Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango alisema kuwa hadi kufikia Juni mwaka 2022, rasimu ya awali ya Sera ya Mifugo itakuwa imekamilishwa na kuwasilishwa ngazi za juu kupata baraka.
“Kumekuwa na kiu kubwa kwa wadau sekta ya mifugo kuona sera ya mifugo yam waka 2006 inafanyiwa mapitio ya utekelezaji ama kufanyiwa marekebisho ili kwendana na mabadiliko ya kijamii, kiuchumi, kiteknolojia na kimazingira yaliyotukumba tangu mwaka 2006” alisema Kaganda.
Kaganda alisema katika kufikia lengo la kufanya mapitio ya sera ya mifugo, Shirika la FAO kwa kushirikiana na Serikili chini ya wizara ya Mifugo na Uvuvi limetoa ufadhili mkubwa ikiwemo kifedha na kitaalamu kwa kufanikisha kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Katibu Tawala mkoa wa Morogoro, Dk Gasper Msimbe alishauri kuwa kenye ukusanyaji wa maoni ya mapitio ya sera hiyo ni vyema kushirikisha wadau mbalimbali wakiwemo watekelezaji wa sera hiyo kutoka halmashauri za wilaya hususani Maofisa Mifugo, idara za ardhi, Maji na wafugaji.