Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dr. Rashid Tamatama afungua Mafunzo ya Wataalamu wa Magonjwa ya samaki

Imewekwa: Sunday 09, December 2018

Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama aliwaeleza Wataalamu wa Magonjwa ya samaki kuwa, tunatakiwa kupambana na kuzuia Magonjwa yanayovuka mipaka ( trans boundary).

Dkt. Rashid Tamatama alizungumza hayo wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa Wataalamu wa Magonjwa ya samaki uliofanyika tarehe 04/12/2018 Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo ulihusisha Nchi 25 duniani na Wataalamu kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, kwa ajili ya Ushirikiano wa Nchi zote kwa pamoja ili kuweza kutambua magonjwa ya samaki yanapotokea.

Katibu Mkuu Dkt. Rashid Tamatama alieleza kuwa, nia yetu ni kuzuia magonjwa samaki, kuyatambua na kuweza kutakabili ni ya aina gani.

Aliendelea Katibu Mkuu (Uvuvi) kueleza kuwa, kwa miaka 2 iliyopita hadi kufikia June 2018 tulizalisha Tan 14,800 za samaki.

‘Tunataka mpaka kufikia mwaka 2020 tuwe tunazalosha tan 30,000’, alisema Katibu Mkuu Uvuvi Dkt. Rashid Tamatama.

Dkt. Tamatama alisema, Nchi yetu inazalisha tan laki 360 hadi 380 kwa Kipindi cha miaka 10 iliyopita na Samak bado hawatoshelezi.

Hata hivyo, tunaweka mikakati ya kuongeza samaki kwa njia ya ufugaji aliendelea kueleza Dkt. Tamatama.

Katibu Mkuu Sekta ya Uvuvi alisema, tunavizimba 386 kwa mwaka huu hivyo uzalishaji wa samaki kibiashara unazidi kuongezeka ukilinganisha na miaka iliyopita.

Naye Dkt. Hamisi Nikuli kutoka Idara ya Uvuvi alisema Sekta hii ni kubwa tunahitaji tupate malighafi ambazo zitasaidia kutoa mazao ambayo yanauzika ndani na Nje ya Nchi.

Lengo la kikao hiki ni kuweka sawa Wataalamu ili kuweza kupambana na magonjwa ya samaki na viumbe vinavyo ishi kwenye Maji, alisema Dkt. Nikuli

.