Katibu Mkuu akisisitiza Uzalishaji wa Malisho ya ng'ombe yenye kuzingatia protini na wanga

Imewekwa: Monday 27, August 2018

KATIBU MKUU MIFUGO ATOA MAAGIZO KWA MAAFISA MIFUGO MKOANI KAGERA.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante Ole Gabriel ametoa Maagizo matatu muhimu kwa maafisa Mifugo mkoani kagera.

Maagizo hayo ni pamoja na:

1.Kutatua/Kushughulikia kero zinazowakabili wafugaji.

2.Kufanya kazi kwa kasi na uhakika wanapo wahudumia wafugaji na kutoa Taarifa kwa Mkurugenzi kwa kuzingatia Majukumu wanayotekeleza kulingana na Ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) ya Mwaka 2015-2020 kama yalivyo ainishwa katika Ibara ya 25 (a)-(Q).

3.Kutoa huduma bora na yenye Viwango,kwani wafugaji wanataka kuona matokea.

.