KAMATI YARIDHIA MAKADIRIO YA BAJETI YA WIZARA 2023/2024

Imewekwa: Monday 27, March 2023

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo imepokea na kuridhia taarifa ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Kamati hiyo ilipokea na kuridhia taarifa hiyo katika kikao cha kupokea na kujadili taarifa ya makadirio ya matumizi ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kilichofanyika jijini Dodoma Machi 27, 2023.

Taarifa hiyo ya makadirio ya bajeti iliyowasilishwa na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mhe. Abdallah Ulega, jumla ni Shilingi Bilioni 292.5, ambapo sekta ya Mifugo fungu 99 ni Shilingi Bilioni 112.1 na Sekta ya Uvuvi fungu 64 ni Shilingi Bilioni 180.5.

Matumizi ya jumla ya fedha hizo ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo na matumizi mengine ya kawaida.

.