Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
KAMATI YA PAMOJA YA UNUNUZI WA MELI YA UVUVI YAKUTANA
KAMATI YA PAMOJA YA UNUNUZI WA MELI YA UVUVI YAKUTANA
Kamati ya pamoja ya manunuzi ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayowakilishwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Sekta ya Uvuvi) na Wizara ya fedha kwa kushirikiana na Serikali ya Japan kupitia kampuni ya Crown agenti imeanza mchakato wa kununua meli kubwa ya kisasa ya kuvulia samaki, gari ya barafu ya kusafirishia samaki pamoja na vyumba vya baridi vya kuhifadhia samaki vitakavyotumiwa na Shirika la Uvuvi Tanzania (TAFICO).
Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi), Dkt. Rashid Tamatamah Septemba 08, 2021 Jijini Dodoma ambapo amesema kuwa mchato huo umeanza baada ya Serikali ya Japan kutoa fedha zaidi ya bilioni 4.2 miaka miwili iliyopita ambayo utengenezaji wa vifaa hivyo utatekelezwa na kampuni ya Sir Lanka.
Amesema baadhi ya mikataba tayari imeshasainiwa na mengine inaendelea kuandaliwa ambapo itasainiwa na Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
“Kamati hii ni kuhusiana na utekelezaji wa mpango wa Uchumi na maendeleo ya jamii (ESDP) ambao ni msaada uliotolewa na Serikali ya japan ambao ulitolewa miaka miwili iliyopita ambapo walitoa bilioni 4.2 za kitanzania kwa ajili ya kununua meli ya kuvua katika ukanda wa uchumi wa bahari kule kusini ambayo ina urefu wa mita 22” amesema Dkt. Tamatamah
Amebainisha kuwa kabla ya kufanya manunuzi kwa kusaini dokumenti za tenda hiyo wamepanga kukubaliana baadhi ya mambo ikiwemo kukubaliana baadhi ya hatua ambazo zitakuwa jumuisho katika ununuzi huo.
“kutokana na changamoto ya covid 19 hata ujenzi wa vifaa hivyo kule nchini sir lanka ambako unaendelea hauendi kwa kasi kama tulivyotarajia kwasababu ni wafanyakazi wachache wanaofanya kazi hivyo itachukua muda lakini tunatarajia hali ikienda sawa ya udhibiti mwakani kuanzia mwezi wa sita na kuendelea tutafanikiwa kupata meli hiyo” amesema Dkt. Tamatamah