Nifanyeje?
- Zipi sifa za kuorodheshwa kama msaidizi wa mtaalam wa mifugo? (Enlisted Paraprofessional Assistant)
- Zipi sifa za kujiandikisha kama mtaalam msaidizi wa mifugo? (Enrolled Paraprofessional).
- Daktari wa mifugo asiye mtanzania (Foreigner) anasajiliwa vipi na Baraza.
- Daktari wa mifugo asiye Mtanzania anaweza kusajiliwa na kufanyakazi hapa nchini? (Temporary and permanent registration)?
DKT. MUSHI AKUTANA NA WAWEKEZAJI TASNIA YA NYAMA NCHINI
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Dkt. Daniel Mushi leo Oktoba 18, 2023 amekutana na wawekezaji upande wa tasnia ya nyama kutoka viwanda vya Elia Food na Tanchoice ambao wamefika ofisini kwake kwa lengo la kujadili namna ya kutatua changamoto ya upatikanaji wa idadi ya mifugo inayopaswa kuchakatwa kwenye viwanda vyao.
Wawekezaji hao walioongozwa na Bw. Rashid, Mkurugenzi wa kiwanda cha Tanchoice kilichopo mkoani Pwani, wameeleza kuwa utoroshaji wa mifugo hai kwenda nchi jirani ni moja ya changamoto kubwa zinazosababisha uhaba wa mifugo nchini ambapo wameweka wazi utayari wao wa kushirikiana na Wizara kwa kutoa taarifa za mianya ya utoroshwaji huo na rasilimali zitakazowezesha doria za kudhibiti changamoto hiyo.
"Lakini Pia ndugu Naibu Katibu Mkuu ili kuwa na suluhu ya muda mrefu ya changamoto hii sisi tupo tayari kuanzisha ranchi ambazo zitazalisha mifugo ya kutosha na yenye ubora ili kukidhi mahitaji ya viwanda vyetu na kwenye hili tumeanza taratibu za awali" Amesema Rashid.
Katika hatua nyingine wawekezaji hao wameishukuru Serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa kuondoa ushuru wa asilimia 80 iliyokuwa ikitozwa kwenye ngozi ghafi inayosafirishwa kwenda nje ya nchi ambapo sasa wameanza kusafirisha kwa kiwango kikubwa badala ya kuteketeza kama walivyokuwa wakifanya hapo awali.
Wakati huo huo Dkt. Mushi amekutana na mmoja wa wawekezaji watarajiwa kwenye sekta ya Mifugo nchini Bw. Musa Hashim ambaye amefika ofisini kwake ili kuweza kupata utaratibu wa kufanya uwekezaji kwenye ranchi na maeneo mengine yaliyopo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi.
"Mwekezaji huyu ni raia wa Somalia anayeishi nchini Denmark na anakusudia kufanya uwekezaji wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 10 hivyo tumemuelekeza akaandike andiko la biashara na kuliwasilisha ili tulipitie na aanze shughuli zake mara moja" Ameongeza Dkt. Mushi.
Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaendelea kukaribisha na kupokea wawekezaji mbalimbali kwa upande wa sekta za Mifugo na Uvuvi lengo likiwa ni kuongeza kiwango cha uzalishaji wa mazao ya Mifugo na Uvuvi nchini.
ReplyForward |