Baadhi ya ng'ombe aina ya Ankole waliopo katika shamba la Alpha Choice -Chato

Imewekwa: Monday 27, August 2018

KATIBU MKUU MIFUGO AKAMILISHA ZIARA YAKE KATIKA MIKOA SITA YA KANDA YA ZIWA.

Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Mifugo) Prof.Elisante Ole Gabriel jana amekamilisha ziara yake ya kutembelea mikoa sita ya kanda ya Ziwa,lengo ikiwa ni kuhamasisha wafugaji kufuga kisasa na kibiashara ili waweze kujikwamua kimaisha.

Malengo mengine yaliyoainishwa katika ziara hiyo ya katibu mkuu ni pamoja na kutambua changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo wafugaji ili ziweze kupatiwa majawabu kama Ilani ya Chama cha mapinduzi (CCM) 2015 -2020 inavyoelekeza katika Ibara ya 25 (a)-(q)

Aidha mikoa sita aliyofanya ziara Katibu Mkuu na kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji ni pamoja na Mwanza,Kagera,Geita,Mara,Simiyu na Shinyanga.

Katika ziara hiyo changamoto kubwa zilizojitokeza ni pamoja na kutokupatikana kwa Mbegu za Malisho,kukosekana kwa Masoko ya mazao ya Mifugo,Kutokuwepo kwa ruzuku ya dawa za mifugo na gharama kubwa ya Mbegu za Uhimilishaji na vifaa vyake.

Katibu Mkuu Mifugo Prof.Elisante Ole Gabriel alizijibu na kuzitolea ufafanuzi changamoto hizo kwa kurejea katika Ilani ya chama cha mapinduzi (CCM) 2015-2020 kama inavyoelekeza namna bora ya kutatua hizo changamoto katika ibara 25 (a)-(q) katika sekta ya mifugo na katika ibara ya 26 na 27 katika sekta ya Uvuvi.

Awali Katibu Mkuu Mifugo alifanya ziara katika kituo cha taifa cha uzalishaji Mifugo kwa njia ya chupa NAIC kilichopo Arusha na kushuhudia shughuli mbalimbali zinazotekelezwa kituoni hapo.

.