TARATIBU ZA KUPATA LESENI ZA UVUVI TANZANIA NA UMUHIMU WAKE

TARATIBU ZA KUPATA LESENI ZA UVUVI TANZANIA NA UMUHIMU WAKE
1. UTANGULIZI Leseni zote za uvuvi Tanzania Bara zinatolewa chini ya Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni za uvuvi za Mwaka 2009. Zifuatazo ni leseni ambazo hutolewa kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake kama ifuatavyo; 

Leseni za kujishughulisha na biashara ya kuuza mazao ya uvuvi ndani ya nchi, 

Leseni za kujishughulisha na biashara ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi.

Leseni za kuingiza samaki na mazao yake nchini 

Leseni za kuvua uvuvi wa kawaida.

Leseni za vyombo vya uvuvi wa kawaida 

Leseni za uvuvi wa burudani (Sport Fishing) 

Leseni za vyombo vya uvuvi wa burudani (Sport Fishing) 

Leseni za Vyombo vya uvuvi wa Kambamiti 

Leseni Maalum (Special Licence/Permit)


UTARATIBU WA KUTOA LESENI HIZI UMEGAWANYIKA KATIKA SEHEMU KUU MBILI (2)
1.1 Leseni zinazotolewa na Halmashauri za Manispaa, Wilaya, Miji (Local Government Authority). 

Leseni za kuvua uvuvi wa kawaida 

Leseni za vyombo vya uvuvi vyenye urefu wa chini ya mita kumi na moja. 

Leseni za kujishughulisha na biashara ya mazao ya uvuvi ndani ya nchi. NB: Pia kufanya usajili wa vyombo vyote vya uvuvi nchini, ila kwa vyombo zaidi ya mita kumi na moja lazima apewe kibali na Mkurugenzi wa Uvuvi nchini.

1.2 Leseni zinazotolewa na Serikali Kuu (Central Government)  Leseni za vyombo vya uvuvi vyenye urefu zaidi ya mita kumi na moja,

Leseni za uvuvi wa burudani (Sport Fishing License) 

Leseni za vyombo vya uvuvi wa burudani (Sport fishing vessel licence)

Leseni za kujishughulisha na biashara ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi. 

Leseni za kuingiza samaki na mazao yake nchini 

Leseni Maalum (Special Licence) 

Leseni za uvuvi wa kambamiti

2. TARATIBU ZA KUPATA LESENI

2.1 Leseni za vyombo vya uvuvi vyenye urefu wa chini ya mita kumi na moja (11) zinatolewa na Serikali ya Mitaa
Nyaraka zinazohitajika ni kama zifuatazo; 

Barua ya muombaji Fomu ya maombi ya usajili wa chombo iliyopitishwa na BMU au Serikali ya kijiji Fomu I (Kanuni za uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 4(1) (4-5). 

Cheti hai cha usalama wa chombo (Valid Certificate of Sea Worthness) kinachotolewa na TASAC, (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 11(1). Form ya maombi ya leseni ya chombo ,Fomu 2(a), Kanuni za uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 11(4). 

Fomu ya maombi ya kuvua (Fomu 3(a)) iliyopitishwa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa, Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(2)(a)
Chombo kilichopatiwa hati ya usajili na kupewa namba, namba hii lazima iandikwe pande zote mbili za chombo kwa gharama za mwenye chombo (kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 7(3) & (4).

2.2 Leseni za vyombo vya uvuvi vyenye urefu zaidi ya mita kumi na moja (>11m) zinatolewa Serikali Kuu Leseni hii inatolewa kulingana na Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 11(2).
Nyaraka zinazohitajika ni kama zifuatazo; 

Barua ya Maombi ya Mteja 

Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa, Jiji (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009,Kanuni 3(4) Fomu ya maombi ya usajili wa chombo iliyopitishwa na Afisa Uvuvi wa Halmshauri za Wilaya au Manispaa, Jiji (Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 4(6). 

Fomu ya maombi ya leseni ya chombo, Fomu 2(a) iliyopitishwa na Afisa uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa, Jiji, (Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 11(4). 

Cheti hai cha usalama wa chombo (Valid Seaworthness Certificate) kutoka TASAC. (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 11(1).  Fomu ya maombi ya kuvua (Fomu 3(a)) iliyopitishwa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya, Manispaa au Jiji, Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(2)(a)

2.3 Leseni za kuvua uvuvi wa kawaida. Leseni hii hutolewa kulingana na Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(1)(a),(b),&(c).
Nyaraka zinazohitajika ni kama zifuatazo;

Fomu ya maombi ya leseni ya kuvua, Fomu 3(a), Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 13(2) (a). 

Barua ya maombi ya mteja 

Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya, Manispaa au Jiji, (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 3(4).Wavuvi ambao vyombo vyao vina urefu wa zaidi ya mita kumi na moja, Barua hii hupelekwa Serikali kuu. Kwa Wavuvi wenye vyombo vilivyo na urefu chini ya mita kumi na moja barua hii inabaki kwa afisa uvuvi wa Halmshauri ya Wilaya, Mji, au Manispaa husika.
NB; - Wageni wote (Non-Citizen) hawaruhusiwi kujishughulisha na shughuli yoyote ya uvuvi katika eneo la maji ya ndani (Territorial waters).


2.4 Leseni za uvuvi wa Burudani (Sport Fishing Licence & Sport Fishing Vessel Licence) Leseni hizi hutolewa na Serikali Kuu Leseni hizi zinatolewa kulingana na Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 18(3)
Nyaraka zinazohitajika ni kama zifuatazo;

Barua ya maombi ya mteja 

Barua ya utambulisho kutoka kwa Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa au Mji, (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009,Kanuni 3(4) Fomu ya maombi ya usajili wa chombo iliyopitishwa na afisa uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa, Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 4(6). 

Fomu ya maombi ya leseni ya chombo, Fomu 2(a) iliyopitishwa na Afisa uvuvi wa Halmashauri za Wilaya, Mji, au Manispaa, Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 11(4). 

Cheti hai usalama wa chombo (Valid Seaworthness Certificate) kutoka SUMATRA. (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 11(1). 

Fomu ya Maombi ya leseni ya kuvua (Fomu 3(a) iliyopitishwa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya, Mji au Manispaa, Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, kanuni 12(2) (a).

Kibali hai cha kufanya kazi nchini (Valid working Permit) kwa muombaji ambae siyo raia wa Tanzania, (Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(2) (b). 

Hati za kuonesha uraia wa muombaji


2.5 Leseni za kujishughulisha na biashara ya mazao ya uvuvi ndani ya nchi, Leseni hizi hutolewa na Serikali za Mitaa Leseni hii inatolewa kulingana na Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(1) (a-c),
Nyaraka zinazohitajika ni kama zifuatazo; 

Barua ya maombi ya mteja. 

Fomu ya maombi ya leseni ya kujishughulisha na biashara ya mazao ya uvuviu, Fomu 3(a), (Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, Kanuni 13(2) (a). Leseni hai ya biashara inayotolewa chini ya Sheria ya kutoa leseni za biashara (Business Licensing Act), Kanuni za mwaka 2009, Kanuni (14).

2.6 Leseni za Kujishughulisha na biashara ya kuuza mazao ya uvuvi nje ya nchi, Leseni hizi hutolewa na Serikali Kuu. Leseni hii inatolewa kulingana na Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009, Kanuni 13(3).

A. Nyaraka zinazohitajika kwa mteja ambae ni Raia wa Tanzania ni kama zifuatazo; 

Barua ya maombi ya mteja 

Barua ya utambulisho kutoka kwa Mkurugenzi/Afisa uvuvi wa Halmashauri za Wilaya au Manispaa au jiji.(Local Government Authority) Barua ya Utambulisho kutoka kwa Zonal Officer Incharge 

Fomu ya Maombi ya leseni ya kujishughulisha na biashara ya mazao ya uvuvi (Fomu 3©) iliyopitishwa na Afisa Uvuvi wa Halmashauri za Wilaya, Mji au Manispaa, Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, kanuni 13(2)(a).  Leseni ya kukusanyia mazao ya uvuvi inayotolewa na Halmashauri za Wilaya au Manispaa, Jiji husika ambako mazao hayo yanakusanywa.  Leseni ya Biashara inayotolewa chini ya Sheria ya kutoa leseni za Biashara (Wizara ya Viwanda,Biashara na Uwekezaji) (Business Licensing Act), Kanuni za Uvuvi za 2009, Kanuni 14.

Tax Identification Number (TIN) 

Tax Clearance Certificate 

Hati ya kuonesha uraia wa Muombaji (Aidha Hati ya kusafiria-Passport au Cheti cha kuzaliwa).

Nyaraka za usajili wa kampuni au jina la Biashara kutoka Brela. i. Kwa Kampuni ambazo ni LTD-inawasilisha Memorandum of Understanding &Article of Association and Certificate of Incorporation, ii. Kwa Kampuni ambazo sio LTD-Inawasilisha Certificate of Registration na Extract from Register iii. Kwa wateja binafsi lazima wasajili Business name ambapo watapewa Certificate of Registration na Extract from Register iv. “Company Status”


NB: Wanahisa wote (Shareholders) na Partiners wote ambao watasomeka katika nyaraka hizi watapaswa kuwasilisha hati ya urai ili kuweza kutambua urai wao.
B. Nyaraka zinazohitajika kwa Mteja ambae si Raia wa Tanzania (Non-Citizen) ni kama zifuatazo;

Mteja ambae si raia wa Tanzania atarusiwa kujishughulisha na biashara ya baadhi ya mazao ya uvuvi ambayo yamegandishwa kama ambavyo ataelekezwa/pata ushauri. Kwani sio kila biashara ya uvuvi ataruhusiwa kufanya. Biashara nyingine ni kwa ajili ya wazawa. 

Mteja huyu atahudumiwa kwa mujibu wa Kanuni za Uvuvi za Mwaka 2009, kanuni 13(18).
Nyaraka Muhimu za kuwasilisha baada ya kupata ushauri ni kama zifuatazo;

Andiko la mradi 

Nyaraka zote za usajili wa kampuni za BRELLA
TRA Certificates. 

Hati za Utambulisho wa Uraia NB: Baada ya andiko kupitiwa na likionekana limekidhi matakwa ya Sekta ya Uvuvi atapewa “No Objection letter” atakayowasilisha TIC. Hivyo baada ya hapo atawasilisha TIC certificate, Work permit & Residence Permit, na nyaraka nyingine na Forms kama ambavyo ataelekezwa.


Wizara inazidi kuwakumbusha wadau wote wa uvuvi kuzingatia matakwa ya Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za Mwaka 2009 pamoja na maboresho yake katika kutekeleza/kujishughulisha na biashara ya samaki na mazao yake nchini. Pamoja tulinde rasilimali yetu ya Uvuvi ili iweze kuwa endelevu kwa kizazi kilichopo na kizazi kijacho.