UTARATIBU WA KUPATA LESENI YA BIASHARA YA MIFUGO HAI

UTARATIBU WA KUPATA LESSENI YA BIASHARA YA MIFUGO HAI

A: BIASHARA YA MIFUGO KATIKA MKOA

Mfanyabiashara anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:

 • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
 • 2.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinatolewa bila malipo
 • 3.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA

Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo ndani ya Mkoa husika. Leseni inatolewa na Ofisi ya Biashara ya Halmashauri kwa malipo ya kuanzia shilingi 80,000 na kuendelea kulingana na ada iliyopangwa na Halmashauri Husika.

B: BIASHARA YA MIFUGO NDANI YA NCHI

Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo ndani ya nchi yaani katika minada ya awali, upili na mipakani anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:

 • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 62,000/-
 • 2.Mkataba wa kupanga ofisi
 • 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA ambacho kinatolewa bila malipo
 • 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA

Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo ndani ya nchi kutoka BRELA kwa malipo ya shilingi 200,000.

Endapo atahitaji huduma nyingine BRELA kama vile

 • 1.Kusajili jina la biashara atalipa kiasi cha shilingi 22,000
 • 2.Kusajili Kampuni malipo yatategemea na kiwango cha mtaji wa biashara ambayo yanaanzia shilingi 160,000 hadi 720,000

C: BIASHARA YA MIFUGO NJE YA NCHI

Mfanyabiashara anayefanya biashara ya mifugo nje ya nchi yaani kutoka minada ya mipakani kwenda nje ya nchi anapaswa kuwa na vielelezo vifuatavyo:

 • 1.Kutambuliwa na kusajiliwa na Bodi ya Nyama kupitia Idara ya Mifugo katika Halmashauri ya Wilaya husika kwa malipo ya shilingi 152,000/-
 • 2.Mkataba wa kupanga ofisi
 • 3.Kuwa na cheti cha Utambulisho wa mlipa kodi TIN kutoka TRA kinachotolewa bila malipo
 • 4.Kuwa na TAX clearance inayokokotolewa TRA

Mfanyabiashara mwenye viambatisho husika atapewa Leseni ya kufanya biashara ya Mifugo nje ya nchi kutoka BRELA kwa malipo ya shilingi 300,000.