Albamu ya Video

  • KIPINDI: (MIFUGO NA UVUVI) UMUHIMU WA DAWATI LA SEKTA BINAFSI

    KIPINDI: (MIFUGO NA UVUVI) UMUHIMU WA DAWATI LA SEKTA BINAFSI

    June 09, 2020

    Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu majukumu na mafanikio ya Dawati la Sekta Binafsi lililo chini ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi lenye lengo la kukuza sekta za mifugo na uvuvi kwa kushirikisha wadau kutoka katika sekta hizo mbili.

  • MATATIZO YA WAFUGAJI SASA YAMEFIKA MWISHO - Waziri Mpina

    MATATIZO YA WAFUGAJI SASA YAMEFIKA MWISHO - Waziri Mpina

    June 09, 2020

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina leo (21/07/2019) amehutubia Wananchi wa Jimbo la Kisesa, Meatu Mkoani Simiyu. Nakusema kuwa, “Matatizo ya Wafugaji sasa yamefika mwisho”.

  • SERIKALI YA AWAMU YA TANO HAINA MCHEZO, WATAWAJIBISHWA - Katibu Mkuu Uvuvi

    SERIKALI YA AWAMU YA TANO HAINA MCHEZO, WATAWAJIBISHWA - Katibu Mkuu Uvuvi

    June 09, 2020

    Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi anayeshughulikia Uvuvi ,Dkt. Rashid amesema Serikali hii ya awamu ya tank haina mchezo! Amesema hayo akiwa Mkoani Rukwa akihutubia Wavuvi wa Wilaya ya Nkasi.

  • KIPINDI: (MIFUGO NA UVUVI) YALIYOTEKELEZWA NA YATAKAYOTEKELEZWA KWA MWAKA 2019/20

    KIPINDI: (MIFUGO NA UVUVI) YALIYOTEKELEZWA NA YATAKAYOTEKELEZWA KWA MWAKA 2019/20

    June 09, 2020

    Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu baadhi ya mambo makubwa yaliyotekelezwa na wizara kwa mwaka 2018/19 na ambayo inatarajia kutekeleza kwa mwaka 2019/20. Kipindi hiki kinatokana na kikao cha Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Mpina alichofanya jijini Dodoma Julai 9 mwaka 2019 kikijumuisha wafanyakazi wote wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi wanaofanya kazi makao makuu ya wizara hiyo na viongozi wa taasisi zilizo chini ya wizara.

  • Wakazi wa Dodoma watoa ya moyoni baada ya kufunguliwa Duka jipya la Nyama/ NARCO

    Wakazi wa Dodoma watoa ya moyoni baada ya kufunguliwa Duka jipya la Nyama/ NARCO

    June 09, 2020

    Wakazi wa Dodoma watoa ya moyoni baada ya kufunguliwa Duka jipya la Nyama/ NARCO

.