Albamu ya Video

  • Msikilize hapa Mkurugenzi Msaidizi wa uratibu wa sera-OFISI YA WAZIRI MKUU, Bi. Devotha Gabriel

    Msikilize hapa Mkurugenzi Msaidizi wa uratibu wa sera-OFISI YA WAZIRI MKUU, Bi. Devotha Gabriel

    June 17, 2020

    Ni kwenye Mkutano uliohusisha wataalam kutoka Wizara za kisekta zinazotekeleza mradi wa ASDP II.

  • KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (ZIARA YA NAIBU WAZIRI ULEGA MKOANI TANGA YAJA NA FARAJA)

    KIPINDI: MIFUGO NA UVUVI (ZIARA YA NAIBU WAZIRI ULEGA MKOANI TANGA YAJA NA FARAJA)

    June 17, 2020

    Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu yaliyojiri katika ziara ya Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega Tanga baada ya kukutana na wadau wa sekta za mifugo na uvuvi mkoani Tanga ambapo ziara hiyo imekuwa na faraja kubwa kwao.

  • Zoezi la Uogeshaji na Kugawa Dawa za Kuogesha Mifugo - Maswa

    Zoezi la Uogeshaji na Kugawa Dawa za Kuogesha Mifugo - Maswa

    June 17, 2020

    Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Luhaga Mpina ashiriki zoezi la kuogesha mifugo na kukabidhi Dawa za kuogeshea mifugo aina ya (Paranex) katika josho la Mwandete Wilaya ya Maswa, Serikali ya awamu ya tano, imejipanga. kuhakikisha changamoto na mateso ya wafugaji yanapigwa marufuku.

  • Mnada wa Maligisu Wilaya ya Kwimba kufutwa! - Waziri Mpina

    Mnada wa Maligisu Wilaya ya Kwimba kufutwa! - Waziri Mpina

    June 17, 2020

    Waziri Mpina akizungumza na Wananchi Wilayani Maswa na kusema kuwa, Mnada wa awali wa Jija urejeshewe haki zake zote kwa kutoingiliwa na wananchi wa Maligisu katika Wilaya ya Kwimba, hivyo watafute eneo sehemu nyingine.

  • https://www.youtube.com/watch?v=bN5Bl8k8hTg

    https://www.youtube.com/watch?v=bN5Bl8k8hTg

    June 17, 2020

    Wizara ya Mifugo na Uvuvi inaandaa mfululizo wa vipindi vya redio na televisheni ambavyo lengo lake kuu ni kutoa elimu na kukufahamisha majukumu ya wizara ya kuboresha sekta ya mifugo na uvuvi kwa mwananchi na taifa kwa ujumla. Katika kipindi hiki utafahamu namna serikali kupitia Wizara ya Mifugo na Uvuvi inavyofanya jitihada mbalimbali kuhakikisha mifugo haifi kwa magonjwa kwa kuweka mipango madhubuti ya wafugaji kuogesha mifugo yao katika majosho kwa kutumia dawa zinazotolewa kwa ruzuku na serikali. Utafahamu mengi zaidi kwa kumshuhudia Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Luhaga Joelson Mpina (Mb) akibainisha hayo wakati wa uzinduzi wa josho lililopo katika viwanja vya nanenane katika Kata ya Nyakabindi, Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu.

.