Maswali Yaulizwayo Mara kwa Mara

NI ​TARATIBU ZIPI ZA KUZINGATIA KWA UVUVI WA KAMBAMITI KWA MSIMU WA MWAKA 2021?

Uvuvi wa Kambamiti kwa msimu wa mwaka 2021 utafanyika kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Namba 22 ya mwaka 2003, Kanuni za Uvuvi za mwaka 2009 na maboresho yake ya mwaka 2020 pamoja na taratibu nyingine ambazo zimeandaliwa na Wizara. Taratibu hizo ni kama zifuatazo: -

 1. Uvuvi wa Kambamiti utafunguliwa tarehe 1 Machi mpaka tarehe 30 Septemba kwa Kanda ya Kaskazini na tarehe 1 Aprili mpaka tarehe 31 Agosti kwa Kanda ya Kusini kila mwaka kwa wavuvi wote wakubwa na wadogo.
 2. Kila muombaji atapaswa kujaza kikamilifu fomu (3b na QA/APP/10) wakati wa maombi kwa kuzingatia Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni zake za Mwaka 2009 na Marekebisho yake ya mwaka 2020.
 3. Maombi ya leseni za uvuvi wa Kambamiti kwa wavuvi wakubwa yatumwe kwa Katibu Mkuu Wizara ya Mifugo na Uvuvi (Uvuvi) na wavuvi wadogo watume maombi katika Halmashauri husika.
 4. Kila chombo kitapata haki sawa. Aidha, utaratibu utakaotumika kuhusu chombo gani kinaanza mwezi machi na chombo gani kitaendelea mpaka mwezi septemba utapangwa na wadau watajulishwa.
 5. Kila Kampuni ya Meli iliyopata kibali cha kuomba leseni itapaswa kuwasilisha ‘Bank Statement’ inayoonyesha uhai wa biashara husika.
 6. Makampuni yanashauriwa kuwekeza katika viwanda vya kuchakata mazao ya Uvuvi, viwanda vya kutengeneza barafu kwa ajili ya kuhakikisha ubora wa mazao ya uvuvi. Aidha, kwa wale ambao watakuwa wameshindwa kuwekeza katika viwanda, wanashauriwa kuwasilisha mikataba ambayo wameingia na wenye viwanda kwa ajili ya kuhifadhia na kuchakata mazao ya uvuvi ili kuhakikisha ubora wa mazao unazingatiwa.
 7. Kwa Makampuni yatakayoajiri wageni, yanapaswa kuwasilisha vibali vya kufanya kazi nchini kwa watu wasio raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 8. Idadi ya meli kwa wavuvi wakubwa zitakuwa kumi na mbili (12) ambapo kila kanda zitaruhusiwa meli nne tu ambapo kutakuwa na mzunguko kwa kanda kila mwezi.
 9. Vyombo vitakavyotumika kwenye Uvuvi wa Kambamiti vitatakiwa kuwa na injini zisizozidi jumla ya nguvu ya Farasi 500 (500HP) na urefu kati ya mita 11.11 hadi mita 25.0, uzito usiopungua tani 20 na usiozidi tani 150 (GRT).
 10. Meli ya uvuvi hairuhusiwi kutumia mnyororo wa kutifua tifua chini (tickler chain) katika Uvuvi wa Kambamiti.
 11. Wavu uwekewe kifaa kisichokamata viumbe adimu kama vile Kasa (Turtle Exclusive Device-TED) na kupunguza samaki wasiolengwa (Bycatch Reducing Device-BRD).
 12. Meli inayokokota wavu nyuma (stern) iwe na wavu mmoja na meli inayokokota wavu ubavuni (outtriggers) iwe na nyavu mbili (moja kila upande).
 13. Chombo cha uvuvi ni lazima kiwe na kifaa kitakachoonyesha mwenendo wa meli ya Uvuvi Baharini (VMS). Gharama za kuweka kifaa cha VMS kwenye meli iwe ni ya mwenye chombo. Aidha, VMs inapaswa kuwashwa muda wote wa chombo kiwapo baharini.
 14. Muda wa kuvua kwa meli utakuwa ni kuanzia saa kumi na mbili asubuhi mpaka saa kumi na mbili jioni.
 15. Eneo la Uvuvi kwa meli zisivue chini ya kina cha mita 6 kulingana na mkataba wa RAMSAR.
 16. Chombo kitakachovua kiwe na ‘Fishing Authorization Certificate’ kutoka nchi ambayo meli hiyo ilikuwa inavua kwa mara ya mwisho.
 17. Chombo kiwe na usajili kutoka TASAC na kupewa Sea worthness certificate.
 18. Chombo kitakachoomba kuvua kitakaguliwa kama hakijahusika kwenye Uvuvi haramu.
 19. Takwimu zitakazowasilishwa wakati wa kushusha mzigo zitathibitishwa na nahodha wa chombo na ‘’Observer wa Idara’’ kwa kusainiwa na wote.
 20. Utoaji wa leseni utazingatia ‘’Kampuni moja meli moja’’ ili kuhakikisha kuwa kila kampuni inamilikiwa na mmiliki tofauti.
 21. Ikiwa itabainika kwamba ‘’Observer’’, Nahodha na ‘’Chief Officer’’ wameshiriki katika kutorosha mzigo au kutoa taarifa zisizo sahihi hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
 22. Idara ya Uvuvi itatoa kibali kwa meli kushusha samaki (bycatch) Bandarini au baharini. Aidha, chombo chochote hakiruhusiwi kumwaga samaki majini.
 23. Chombo chochote hakiruhusiwi kuchafua mazingira kama vile kutupa takataka ngumu (Plastics), Mafuta na uchafuzi mwingine unaofanana na huo.
 24. Meli zitakapokuwa zinavua kwenye kanda husika zifanye mawasiliano na Serikali ya Kijiji/Mtaa, mara watakapofika kwenye eneo lao na watoe taarifa wakati wanaondoka na kulipa ushuru stahiki.

Sifa gani za mtaalam kusajiliwa kama daktari wa mifugo?

Awe ana shahada ya kwanza ya tiba ya mifugo (BVM) kutoka katika chuo kinachotambuliwa na Baraza kwa ada ya TZSh. 50,000/= na endapo amesomea nje ya nchi atahitajika kwanza kufanya na kufaulu mtihani wa Baraza

How to establish a cage Fish Farm


The following steps are proposed to obtain a license to establish a cage fish farm:

 • The prospective farmer and investor will start by visiting responsible fisheries agencies such where the proposed cage culture investment is to be established to obtain information on the requirements and expectations.
  • At this stage, the farmer and investor are expected to either prove that they are citizens of the respective countries by presenting authentic and valid national identity cards or documents to prove that they are legally living in the countries for foreign investors.
  • In addition, foreign investors are expected to present an investment license issued by respective investment authorities.
 • Site suitability report done by the above mention competent authorities
 • The prospective investors or farmers who want to establish intensive or semi-intensive aquaculture production systems like cage aquaculture shall submit to the competent authority for approval, a plan of the establishment including projectionand operation details of the farm in line with the above mentioned in these guidelines with the following information. The names and address of the establishments and managers; The type of aquaculture to be practiced;
 • The water discharge plan including measures for treatment of farm effluents into the surroundings and steps for screening to avoid farmed fish escapees;
 • The clearance/permit for water abstraction and discharge in case of use in excess of 400m3 of water a day;
 • Evidence of community involvement and Social cooperate responsibility near the site (land free of encumbrances).
 • Certificate of incorporation and registration of business
 • Registration with local government/ trading license
 • Directorate of Aquaculture permit issued
 • Evidence of feed being obtained from a certified source(s)
 • Evidence of seed being obtained from a certified source(s).

If these requirements are met, the farmers will be issued a two year provisional license to establish and operate a cage fish farming enterprise.At this stage, the farmer can establish a cage fish farm on the approved site.Approved applicants are given approval numbers, and are added to the list of certified aquaculture establishments authorized to produce and sale particular aquaculture products locally and/or externally if they meet the export market requirements. Applications shall periodically be newed whenever major changes are made to the originally approved plan. During operation and establishment, farmers or investors are expected to comply with all policies related with cage fish farming (Table 4-6). The respective fisheries agency will monitor farm operations and compliance through the first two years and if satisfactory, an operating license for a longer period shall be issued.

However, establishment and operating licenses for cage fish farming on Lake Victoria shall not be offered for more than ten successive years.

Namna gani nitaanza ufugaji wa samaki.

Namna ya kuanza ufugaji bora wa samaki:

1.Andaa eneo lenye ukubwa usio pungua robo heka sehemu salama.

2.Wasiliana na Mkurugenzi wa uzalishaji viumbe samaki kupitia Katibu Mkuu wa Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

3.Utapewa darasa kadri itakavyo pangwa...............

Aina ya Uvuvi na Nyavu zisizotakiwa.

UVUVI WA NYAVU (RING NET)

Uvuvi wa nyavu zijulikanzo kama RING NET unaovuliwa "MCHANA" upigwe marufuku.

Kisheria uvuvi huu wa mchana wavuvi hawafuati sheria walio wekewa na idara ya uvuvi.

 1. Wanavua kina cha maji mita (7) hadi (10) badala ya mita (50) na zaidi.
 2. Kuwa uvuvi hu wa mchana wavuvi wote hutumia chupa za Gesi (5).
 3. Hawaiheshimu mitego ya watu wengine.
 4. Samaki wa kuvuliwa mwezi mmoja wao wanavua kwa siku mmoja.
 5. Uvuvi huu wa kuvua wa kuwafukuza samaki una madhara makubwa ya kuwahamisha samaki na kutoweka katika maeneo hayo
ADHABU

Faini milioni tano au kifungo cha miaka mitatu au vyote na mtego na chombo kifilisiwe
na mtego huu utekelezwe.

KOKORO
Mvuvi yeyote atakae kamatwa anavua kokoro kwa kuzingatia kuwa kokoroni uvuvi unao
haribu mazalia ya samaki na kuua samaki wachanga. Adhabu yake iwe miaka iwili jela,

faini milioni tatu,mtego na chombo vifilisiwe na mtego uteketezwe.

NYAVU ZA KUTEGA
Nyavu za kutega zianzie nchi mbili na nusu na kuendelea.

Utoaji wa Leseni ya Uvuvi

Kwa mujibu wa Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya Mwaka 2003 na Kanuni za Mwaka 2009, utoaji wa leseni za uvuvi chini ya mita 11 hutolewa na Halmashauri husika na vyombo vinavyozidi mita 11 hutolewa na Wizara. Leseni hii hutumika kuanzia Januari hadi Desemba. Aidha, Halmashauri ndizo zinazohusika na usajili wa vyombo vyote vinavyoruhusiwa kuvua ikiwa moja ya vyanzo vyake vya mapato. Ukaguzi na utoaji wa Cheti cha Usalama wa Chombo (Seaworthness Certificate) ni jukumu la Mamlaka ya Usalama wa Vyombo vya Usafiri na Nchi Kavu na kwenye Maji (SUMATRA) chini ya Wizara ya Uchukuzi.

Ili kuondoa tatizo la ucheleweshaji wa utoaji wa leseni na usajili wa vyombo vya uvuvi, Wizara kwa kuanzia imechukua jukumu la kushirikiana na Halmashauri za Manispaa za Temeke, Ilala na Kinondoni za Mkoa wa Dar Es Salaam kwa kuanzisha mfumo wa kutoa leseni za papo kwa papo, kusajili vyombo na kutoa tagi maalum (Smart License). Zoezi hili litasaidia upatikanaji wa leseni za uvuvi kwa wakati na kuongeza mapato kwa Halmashauri. Kutokana na mafanikio ya zoezi hili, Wizara itaendelea kutoa elimu na kuhamasisha Halmashauri nyingine zifuate mfumo huu ambao unatarajiwa kujumuishwa kwenye Sheria ya Uvuvi.

.